Siri ya Aman Karume, Maalim Seif yafichuka

10 02 2010

•  Yabainishwa walitishiwa kushtakiwa The Hague

SIRI ya mapatano ya ghafla kati ya Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, yanayoelekea kuzaa serikali ya mseto visiwani, imefichuka.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na Tanzania Daima Jumatano, umebaini kuwa chanzo cha makubaliano ya ghafla ya viongozi hao imetokana na shinikizo kutoka nchi za Jumuiya ya Ulaya zilizotishia kuwafikisha katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), The Hague nchini, Uholanzi viongozi hao kama damu itamwagika tena katika uchaguzi mkuu ujao.

Tayari marais na viongozi kadhaa wa siasa barani Afrika, wamefikishwa katika mahakama hiyo kujibu tuhuma zinazowakabili za kusababisha umwagaji damu katika nchi zao.

Hadi kufikia Oktoba mwaka jana, nchi 110 zilisaini kukubali na kuitambua mahakama hii, ikiwemo Tanzania.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa hadi sasa mahakama hiyo iliyoanza kutekeleza majukumu yake Julai Mosi 2002, The Hague nchini Uholanzi, imefungua uchunguzi katika maeneo manne ya Uganda Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Afrika ya Kati na katika jimbo la Darfur.

Hadi sasa imewafikisha kizimbani watu wanaokadiriwa kufikia 10, saba wamebakia kama washtakiwa, wawili wanaaminika kuwa wamefariki dunia, wanne wako chini ya ulinzi na mmoja anatakiwa kuonekana kwa hiari mbele ya mahakama hiyo.

Kwa upande wa Afrika wapo viongozi wakuu kadhaa ambao mashtaka yao yamefikishwa mbele ya mahakama hii na kesi zao bado hazijaisha, akiwamo aliyewahi kuwa Rais wa Liberia, Charles Taylor; Makamu wa Rais wa zamani wa Kongo, Jean Pierre Bemba; na sasa anasakwa Rais wa Sudan, Omar al-Bashir

Mbali na hao wapo wapiganaji wa DRC waliofikishwa ICC ambao ni Thomas Lubanga, Germain Katanga na Mathieu Ngudjolo Chui.

Nchi ambazo hivi karibuni zimeingia kwenye machafuko, viongozi wake wako katika hatari ya kufikishwa ICC, ni Kenya na Zimbabwe ambapo majina ya baadhi ya watuhumiwa waliohusika katika vurugu za uchaguzi, yamekwishafikishwa katika mahakama hiyo.

Mbali ya Kenya na Zimbabwe, nchi nyingine kadha wa kadha zimekuwa zikitajwa ikiwemo Zanzibar kwamba baadhi ya viongozi wake, wanaweza kufikishwa ICC kutokana na matendo yao yaliyosababisha umwagaji wa damu wakati wa uchaguzi.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na baadhi ya viongozi waandamizi wa CUF, vilisema Maalim Seif na Rais Karume, waliwahi kuitwa na nchi za Jumuiya ya Ulaya na kupewa onyo kwamba kama damu itamwagika tena Zanzibar wakati wa uchaguzi mkuu ujao, watafikishwa katika mahakama hiyo kujibu tuhuma za mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Tangu kumalizika kwa uchaguzi huo visiwani Zanzibar, Maalim Seif amewahi kukaririwa akisema atakwenda kuishtaki serikali ya Rais Karume kwenye Jumuiya ya Nchi za Ulaya ambako inasemekana alipata ushauri wa kumtambua Rais Karume.

Duru za kisiasa kutoka visiwani humo zinadai kuwa baada ya kupewa tahadhari hiyo, viongozi hao waliamua kukutana katika Ikulu ya Rais Karume Zanzibar kwa mara ya kwanza baada ya miaka tisa ya uhasama wa kisiasa na kuamua kumaliza tofauti zao bila kuvishirikisha vyama vyao.

Viongozi hao wenye historia kubwa katika visiwa vya Zanzibar, pia walipeana mikakati ambayo hadi sasa imebaki kuwa siri kuhakikisha wanajenga mazingira mazuri ya kufanyika kwa uchaguzi huru na wa haki visiwani humo.

Mara baada ya mkutano wa viongozi hao, Maalim Seif, ambaye amepata kuwania kiti cha urais wa Zanzibar mara tatu mfululizo na kushindwa, alitangaza kumtambua Rais Karume.

Hali hiyo imezua mjadala mzito na imemuweka Maalim Seif katika wakati mgumu hasa alipofanya mkutano wa hadhara siku mbili baada ya kukutana na Rais Karume katika Ikulu ya Zanzibar.

Katika mkutano huo, wapo waliompinga Maalim Seif kwa kumzomea na kumwita msaliti, huku kina mama wakiangua kilio na kueleza mawazo ya kutokuwa na imani naye.

“Watu wanajiuliza imekuwaje ghafla Maalim Seif anamtambua Karume, mara bila hata ridhaa ya chama, anawatangazia wanachama, huku Rais Karume anafanya uteuzi wa wajumbe wawili wa Baraza la Wawakilishi kutoka CUF?

“Hii yote ni kutokana na kibano walichokipata na ndio maana hata ukiwauliza, ‘Kwenye kikao chenu cha faragha, mlikubaliana nini? Nani alimwita mwenzake?’, hakuna mwenye majibu,” alisema mmoja wa wanasiasa wenye ushawishi mkubwa visiwani Zanzibar,” alisema.

Kwa mujibu wa habari hizo, wadadisi wa mambo ya kisiasa wanaamini kuna msukumo kutoka nje kwani msimamo wa CUF awali ni kwamba walipinga Azimio la Butiama lililotolewa na Halmashauri Kuu ya CCM, Machi mwaka jana la kutaka Serikali ya Mseto ianzishwe mwakani.

CCM walitaka mseto uanze baada ya uchaguzi mkuu mwakani, lakini CUF wakataka uanze sasa.

Wakati mvutano huo ukiendelea kulijitokeza hoja ndani ya CCM kwamba yatafutwe maoni ya Wazanzibari wote kuhusu suala hilo kwa kuwa Zanzibar si ya CCM wala CUF pekee.

Akizungumzia kuhusu tishio la kufikishwa katika Mahakama ya The Hague, Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano visiwani Zanzibar CUF, Salum Biman, alisema hakuna shinikizo lolote kutoka nje lililosababisha Rais Karume na Maalim Seif kufikia muafaka.

“Maneno hayo yanasemwa, hata sisi tunaambiwa hivyo, lakini ukweli unabaki kwamba viongozi hao wamezingatia maslahi ya Wazanzibar,” alisema.

“Mimi nafikiri kama kiongozi wa kupelekwa The Hague ni Rais mstaafu Benjamin Mkapa ambaye mwaka 2000 hadi 2001 yalipotokea machafuko na watu zaidi ya 40 kuuawa, alikuwa Amiri Jeshi Mkuu,” alisema Biman.

Kuhusu uchaguzi mkuu ujao visiwani Zanzibar pamoja na uanzishaji wa Serikali za Mseto, duru za siasa zinasema kuwa CUF wamefanikiwa kutimiza malengo yao hasa ya kutaka uchaguzi mkuu mwaka huu uahirishwe.

Wachambuzi wa mambo ya siasa visiwani humo, wanasema kuwa ingawa hoja ya Maalim Seif awali ilikuwa kutaka uchaguzi mkuu uahirishwe, lakini uchaguzi katika visiwa hivyo, unaweza kuahirishwa kutokana na kuwapo kwa muda mfupi wa kufanya mabadiliko ya Katiba ili suala la Serikali ya Mseto, liingizwe kwenye Katiba ya Zanzibar.

Akizungumzia suala hilo, Mwanasheria Ali Ali wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa SMZ, alisema kama viongozi wa CUF na CCM wana dhamira ya kweli, Zanzibar wanaweza kufanya uchaguzi mwaka huu.

Alikiri kuwa licha ya kuwapo kwa muda mfupi, anaweza kuitisha vikao vya dharura vya Baraza la Wawakilishi na kufanya mabadiliko ya Katiba yatakayokidhi matakwa ya Serikali ya Mseto.

Wiki mbili zilizopita, Baraza la Wawakilishi lilipitisha hoja binafsi ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Abubakar Khamis Bakari, ya kutaka kuundwa kwa Serikali ya Mseto ili kujenga umoja na maridhiano kwa Wazanzibari ambao wamekuwa katika migogoro ya kisiasa kwa muda wa zaidi ya miaka 15.

Wajumbe wa baraza hilo wote kwa sauti moja walikubaliana na suala hilo kwa kuridhia baaada ya Baraza la Wawakilishi kuwasilisha mapendekezo ya hoja binafsi ya Chama cha Wananchi CUF na kujadiliwa na mwakilishi huyo wa jimbo la Mgogoni Pemba.

Hata hivyo kabla ya kufanyika kwa mabadiliko hayo CUF walikubali kufanya mabadiliko katika hoja kadhaa baada ya wajumbe wa CCM kutaka kufanyiwa mabadiko hayo ya hoja yake.

Marekebisho hayo ni pamoja na hatua ya kutaka ridhaa ya wananchi kwa njia ya kura ya maoni, na marekebisho ya Katiba endapo wananchi wataridhia uanzishwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa. Mambo yote hayo yafanywe kabla ya uchaguzi mkuu mwaka huu.

Wakati huo, Maalim Seif yuko nchini Uingereza ambapo pamoja na mambo mengi anatarajia kufanya mkutano na Wazanzibari waishio huku, kuwajulisha dhamira mpya ya kumtambua Rais Karume na uundwaji wa Serikali ya Mseto Zanzibar.

Hatua hiyo ni mwendelezo wa harakati zake za kufanya ushawishi wa ndani na nje lengo likiwa kutafuta uungwaji mkono wa muafaka wake na Rais Karume.

Taarifa ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata, zilisema kuwa Maalim Seif, anatarajia kufanya mkutano huo Februali 13, katika Ukumbi wa Durning Hall, jijini London, kueleza sababu na hatua ya maridhiano yaliyofikiwa kati yake na Rais Karume.

Taarifa za mkutano wa Maalim Seif nchini Uingereza, zilithibitishwa pia na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CUF visiwani Zanzibar, Biman.

Alisema Maalim Seif atakuwa na mikutano mbalimbali ya kimataifa ambayo hakuifafanua na pia atafanya mikutano na Wazanzibari waiishio huko.

“Kweli yupo nchini Uingereza kwa ajili ya mikutano yake ya kimataifa. Atazungumza mambo mengi mojawapo kuwaeleza hatua ambayo tumefikia katika maridhiano yetu,” alisema Bimani.

Jumuiya ya Wazanzibari waishio Uingereza (ZAWA) kupitia mtandao wa Jamii Forum umewakaribisha raia wote waishio nchini humo na nchi za karibu, kuhudhuria mkutano wa Maalim Seif.

“Wazanzibari wote, wake kwa waume, walioko Uingereza na nchi za jirani wanakaribishwa kuhudhuria. Huu ni mkutano wa kihistoria na wa kwanza kufanyika London baada ya makubaliano yaliyofikiwa baina ya CUF na CCM Zanzibar,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo

Advertisements

Actions

Information

One response

9 03 2010
Fatma

Jamani hii post haikutoka vizuri. Please publish it again.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s
%d bloggers like this: