Kili Stars yalala, Zanzibar yafanya mauaji

1 12 2009

Michael Momburi, Mumias
TANZANIA imetupa karata yake ya kwanza kwenye michuano ya Chalenji mjini Mumais jana kwa matokeo ya furaha na uzuni kutoka kwa timu zake za Zanzibar Herous kuisambarati Burundi 4-0, huku Kilimanjaro Star wakilala kwa mabao 2-0 kutoka kwa mabingwa watetezi Uganda.
Bao la mapema lilofungwa kwa kichwa mshambuliaji Owen Kasule akiunganisha krosi ya Godfrey Walusimbi dakika ya 2 ya mchezo lilitosha kuichanganya Kilimanjaro Stars walionekana kupwaye zaidi kwenye nafasi ya kiungo kabla ya Mike Serumaga kufunga bao la pili dakika 88.
Viungo Tony Maweje na Senyonjo wa Craines alitawala sehemu ya kati na kuwachanganya kabisa Shabani Nditi, Juma Nyoso na kuwafanya wasionekana kabisa.
Beki Nyoso alitolewa nje kwa kadi mbili za njano baada ya kumchezea vibaya Senyonjo huku awali akiwa ameunawa mpira makusudi hivyo kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Vita kuu katika mchezo huo ilikuwa ni kwenye winga ambao upande wa kushoto Juma Jabu alikuwa na kibarua cha kumzuia Danny Wagaluka, huku Shadrack Nsajigwa wakionyeshana na Steven Bengo wote ni wachezaji ya Yanga.
Kili Stars iliuanza mchezo huo kwa kujilinda zaidi jambo lilokosesha amani kocha Marcio Maximo ambaye alikuwa akipiga makelele ya kuwawata wachezaji wake wasogee mbele.
Mshambuliaji kinara wa ufungaji katika Ligi Kuu ya Tanzania, Jonh Bocco alikuwa chini ya ulinzi mkali wa mabeki wawili Andy Mwesigwa na Joseph Owino wa Simba.
Kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Henry Joseph na aliingia kuchukua nafasi ya Nditi, huku Mrisho Ngasa akichukua nafasi ya Boko wakijaribu kuongeza kwenye shambuliaji.
Uganda ambao ni mabingwa mara 10 wa michuano hiyo wakitumia vizuri maumbo yao makubwa na urefu kuzuia pasi zote za juu na chini ambao kipa Mohamed Mwarami alikuwa akijaribu kutumia kuanzisha mashabulizi ya kushitukiza.
Kipindi cha pili washambuliaji Mrwanda na Ngasa wakitumia kasi yao kujaribu kichanganya ngome ya Uganda bila ya mafanikio. Beki Jabu alipewa kadi ya njano kwa kumkwatua Wagaluka.
Star wakionekana wanahamu kubwa ya kutafuta bao la kusawazisha kwa nguvu walijikuta wakifungwa bao la pili kwa mpira wa adhabu uliopigwa na Serumanga na kwenda moja kwa moja wavu na kumwacha Mwarami asijue la kufanya.
Mapema, pamoja na baridi kali na mvua iliyokuwa ikinyesha mjini humo haikuizia Zanzibar kuichakaza Burundi kwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza kwa Kundi C uliochezwa mjini Mumias.
Zanzibar walifungua kalamu ya mabao dakika ya 15 lilofungwa na Agrey Moris akiunganisha krosi ya Nadir Haroub ‘Canavaro’ dakika moja baadaye beki wa Burundi, Hassan Hakzmana alijifunga mwenye akijaribu kuokoa mpira uliokuwa ukienda golini kwake.
Vijana wa Karume wakionyesha wamedhamiria kupata matokeo mazuri kwenye mechi hiyo waliandika bao la tatu dakika 22 lilofungwa na Mohamed Salum kabla ya Nzeyimana Hussein kujifunga bao la nne dakika 70 na kuicha Intamba Burundi wasijue nini kinachoendelea uwanja hapo.
Kocha wa Zanzibar, Hemed Moroco aliwasifu wachezaji wake wa kucheza soka ya kujituma na kuelewana na kufanikiwa kupata ushindi huo wa kishindo.
Mjini Nairobi, Rwanda walifaidika na bao la mapema la kujifunga wenye Somalia kupata ushindi wa 1-0.
Leo michuano hiyo inaendelea kwenye uwanja wa Nyayo Jijini Nairobi kwa mchezo mmoja baina ya Ethiopia na Djibout.
Katika uwanja wa Mumias mjini hapa timu za kundi C, Kilimanjaro Stars, Zanzibar, Uganda na Burundi zitakuwa mapumzikoni kwa kuendelea na mazoezi.
Kilimanjaro Stars itakuwa ikijianda na pambano lake dhidi ya ndugu zake Zanzibar mchezo ambao umeanza kuibua hisia nyingi kwa kila mmoja kumhofia mwenzake. Timu hizo ambazo zimepiga kambi kwenye hosteli moja zimekuwa zikihofiana na wachezaji na viongozi wake hawashirikiani kwa kina kama inavyokuwa katika michuano mingine.
Michuano ya Chalenji inaendelea mjini hapa, lakini imekuwa na msisimko mdogo huku mashabiki wengine wakiwa hawana taarifa kabisa ya nini kinaendelea.
Kikosi cha Kilimanjaro Stars, Mohamed Mwarami, Shedrack Nsajingwa, Juma Jabu, Kelvin Yondani, Salum Sued, Juma Nyoso, Danny Mrwanda, Shabani Nditi, Jonh Boko, Kigi Makasi na Nurdin Bakari. Akina benchi, Shaban Kado, Henry Joseph, David Naftari, Jerry Tegete, Musa Mgosi, Mrisho Ngasa na Mwaipopo.

Chanzo: Mwananchi 29 Nov 2009

Advertisements

Actions

Information

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s
%d bloggers like this: