Muswada wa kutenga siasa, biashara wagubikwa na utata

19 10 2009

Na Joyce Mmasi

MUSWADA wa maadili ya uongozi itakayotenga siasa, biashara na matumizi ya fedha wakati wa uchaguzi unaotarajia kupelekwa bungeni mwanzoni mwa mwaka ujao, umeonekana kuwa mgumu kutekelezeka kutokana na utata katika utekelezaji baadhi ya vipengele vyake. Sehemu kubwa ya muswada huo unaogusa nafasi ya wafanyabishara katika siasa, pia unawataka wanasiasa pamoja na vyama vyao kutaja viwango vya pesa watakavyotumia katika uchaguzi.

Wiki iliyopita akihutubia maadhimisho ya miaka 10 ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Rais Jakaya Kikwete, alisema serikali itahakikisha maadili ya uongozi yanarejeshwa pamoja na kulinda na kudumisha umoja wa kitaifa. Kikwete alisema katika kulinda maadili, serikali imeandaa miswada ya maadili ya uongozi itakayopelekwa bungeni mwanzoni mwa mwaka ujao kuzuia rushwa katika uchaguzi na kuwadhibiti wafanyabiashara ambao wamekuwa wakikimbilia katika siasa ili kujinufaisha kibiashara.

Rais Kikwete alifafanua kwamba, wakati wa Azimio la Arusha, ilikuwa rahisi kwa Mwalimu Nyerere kusimamia maadili ya uongozi, jambo ambalo ni vigumu hivi sasa na akasisitiza ni lazima kuwe na namna ya kusimamia maadili ya uongozi.

Hata hivyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Sera), Philip Marmo, aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa muswada utakaojadiliwa utahusu matumizi ya fedha wakati wa uchaguzi. Alifafanua kwamba, muswada huo umebebwa na mambo mengi yakiwemo kudhibiti fedha kutoka kwa wafadhili walioko nje ya nchi. Marmo aliongeza kwamba, katika muswada huo mpya hakuna nia ya kuwabana wafanyabiashara kwa kuwa kwa kufanya hivyo itakuwa ni kuvunja katiba ya nchi.

“Sio kweli kuwa ukiwa mfanyabiashara hutakiwi kugombea nafasi yoyote ya uongozi; kwa kuwa mfanyabiashara haina maana kuwa wewe sio raia wa Tanzania. Tunachozingatia katika muswada huu ni matumizi ya fedha wakati wa uchaguzi ambao utawahusu wabunge wote wa viti maalum, wa kuchaguliwa, vyama vya siasa na wagombea urais,” alisema Marmo.

Akifafanua, Marmo alisema katika muswada huo, mgombea wa nafasi yeyote anapaswa kuweka wazi kiasi cha fedha atakazotumia katika uchaguzi, aeleze kimepatikanaje na endapo ni halali na kwamba endapo mhusika atazidisha kiasi alichoeleza atapaswa kueleza ni kwa nini na alipozipata.

Naye Sadick Mtulya anaripoti kuwa, baadhi ya wabunge kutoka Zanzibar wamesema hatua hiyo ni nzuri lakini inahitaji nia ya dhati ya matendo katika utekelezaji wa sheria hizo. Rais Kikwete ambaye mwanzoni mwa mwaka huu alizungumzia kuhusu viongozi kuchagua siasa ama biashara.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Actions

Information

One response

19 10 2009
zirppo

Hivi kweli ni vigumu hivi leo kwa kiongozi wa nchi kusimamia maadili ya uongozi? Na hii hasa inamaanisha nini ikiwa kiongozi mwenyewe anashindwa kusimamia maadili ya uongozi? Sisi wananchi wa kawaida tuitafsiri vipi kauli hii? Mimi naamini kwa dhati kabisa kuwa Rais Kikwete hawezi kutoa kauli kama hii.

Hata hivyo, kwa maoni yangu, jambo la msingi kabisa hapa sio tu kuwa kuna haja na ulazima wa kusimamia maadili ya uongozi, lakini kuna umuhimu mkubwa wa kutenganisha siasa na biashara. Na hivyo ndivyo alivyokuwa akipigania Mwalimu. Kwa lugha nyepesi, mwananchi yoyote yule anayetaka kugombea nafasi ya uongozi katika chama au serikali, basi lazima achaguwe moja; aendelee kuwa mfanya biashara au awache mara moja shughuli za kibiashara ikiwa ataamua kujitosa katika siasa. Hawezi kufanya yote mawili kwa wakati mmoja. Kuruhusu hali hiyo iendelee ndiyo sawa na kupalilia mizizi ya ufisadi, rushwa na hata wizi wa mali za serikali.

Kwa hivyo, muswada lazima uwe na nia ya kuwabana kwa makusudi kabisa wafanya biashara wanaotaka kujitosa katika siasa. Kwani nani kasema kuwa ukiwa raia hupaswi kufuata kwa vitendo maadili ya uongozi?

Muhammad Yussuf
Interim Executive Director
Zanzibar Institute for Research and Public Policy
P.O. Box 416
Zanzibar
TANZANIA
Tel: 0777 707820 Cellular
Tel: 0242 233526 Office
Email: yussufm@gmail.com
Weblog: http://www.zirppo.wordpress.com

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s
%d bloggers like this: