Nyumba ya kada wa CCM Pemba yalipuliwa kwa bomu

3 10 2009

Na Salma Said, Wete Pemba

MLIPUKO mkubwa umetokea katika nyumba moja huko Wete,Kaskazini Pemba, siku moja baada ya Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, kuwahakikishia wananchi na wageni kuwa hali ya usalama Zanzibar, ni shwari.

Mlipuko huo ulitokea saa 4:00 usiku wa kuamkia katika nyumba inayomilikiwa na kada wa CCM, Ramadhan Issa Kipaya, iliyoko katika Mtaa wa Mtemani, wilayani Wete.

Ingawa mlipuko huo umesababisha kuta za nyumba kuharibika, lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa.

Habari za awali zilisema kada huyo ni miongoni mwa wahamasishaji wakubwa wa wanachama wa CCM wanaoogopa kujitokeza ili kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura, kisiwani Pemba.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Yahya Rashid Bugi alithibitisha kutoka kwa mlipuko huo, uliotokea wakati watu wengi wakiwa majumbani mwao.

“Ni kweli mshindo ulikuwa mkubwa sana na watu nyakati hizo walikuwa wamelala, mimi nilikuwa nyumbani naangalia televisheni lakini niliposikia, nikatoka na kwenda katika eneo la tukio tukiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba,” alisema kamanda Bugi.

Alisema mlipuko huo umetokana na bomu lililotengenezwa kwa baruti ambalo hutumika kwa kupasulia miamba ya baharini na nchi kavu hasa katika utengenezaji wa barabara.

“Haya mabomu hutengenezwa kwa baruti lakini huwa yanapasua miamba ya baharini na na nchi kavu pia, hutumiwa na watengenezaji wa barabara na mlio wake unakuwa mkubwa kama mabomu ya kawaida,” alisisitiza.

Kwa mujibu wa Bugi mabomu hayo ni sawa na yale yaliolipuliwa hivi karibuni katika madaraja ya Piki, wilayani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dadi Faki Dadi, alisema ulipuaji wa mabomu hayo unafanywa na wanachama wa CUF ambao hawataki kuona wananchi wanajitokeza na kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura.

Dadi alisema pamoja na kuwa na uhakika kuwa vitendo hivyo vya uharamia vinafanywa na wafuasi wa CUF, lakini hawatawachukulia hatua za kuwakamata kwa kuhofia kwenda kuwalisha chakula cha bure, ambacho kitaigharimu serikali ya mapinduzi Zanzibar.

Juzi akiwa katika ziara yake ya ziku mbili Kisiwani Pemba, Rais Karume amewahakikishia wananchi na wageni wanaotaka kutembelea Zanzibar, kuwa hali ya usalama katika visiwa hivyo ni shwari na kwamba hakuna matatizo kama inavyokuzwa na waandishi wa habari.

Alisema tangu miaka ya nyuma, Zanzibar ni nchi ya amani na utulivu na kwamba mtindo wa hivi karibuni wa watu wasiojulikana kuchoma moto nyumba, hauna maslahi kwa wananchi.

“Zanzibar kuna amani tena utulivu wa kutosha, watu wanafanya shughuli zao za kawaida na tunawalika wengine pia waje kutembelea visiwa hivi,wachane na wale wanaosema kuwa Zanzibar hakukaliki, nyumba zinalipuliwa hayo ni maneno ya waandishi tu,” alisema Rais Karume.

Uandikishaji wa daftari la kudumu la wapigakura unaoendelea katika Mikoa mwili Kaskazini Unguja na Kaskazini Pemba umekuwa na matukio ya kila yakiwemo yanayoashiria kuvunja amani.

Chanzo: Mwananchi la 30 Oktoba 2009

Advertisements

Actions

Information

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s
%d bloggers like this: