CUF yaichongea Tanzania Jumuiya ya Ulaya

3 10 2009

Salma Said, Wete Pemba

CHAMA Cha Wananchi (CUF), kimeanza kuishawishi Jumuiya za Ulaya (EU), ili iwekee vikwazo Tanzania, kufuatia matatizo yanayojitokeza katika uandikishaji wa wananchi katika Daftari la Kudumu la Wapigakura, visiwani Zanzibar.

Tayari Mkurugenzi wa uchaguzi katika chama hicho, Mhene Said Rashid, yuko jijini Stockholm,Sweden, kuanza ushawishi kwa Jumuiya ya Ulaya, kuibinya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar, kwa madai kuwa haziheshimu demokrasia.

Habari zilisema mjumbe huyo, anatarajiwa kutembelea Finland, Sweden na Denmark na kukutana na maafisa wa jumuiya hiyo na kuzungumza nao kuhusu vitendo vya kutoheshimika kwa misingi ya demokrasia nchini Tanzania.

Akizungumza kutoka Stockholm jana, Rashid alisema lengo la safari yake katika nchi hizo ni kuzishawishi nchi zinazoifadhili Tanzania, ziache kuisaidia kwa madai kuwa haiheshimu misingi hiyo.

Alisema hali hiyo inadhihirishwa na kitendo cha kuwanyima haki yao ya kuandikishwa, wananchi wa Zanzibar kwa madai kwamba hawana vitambulisho ya ukazi wa visiwa hivyo.

“Tuna matatizo ya uandikishaji wa wananchi katika Daftari la Kudumu la Wapigakurana, Watu hawaandikishwi kwa sababu wengi hawana vitambulisho. Daftari hili ndilo litakalotumika katika upigaji kura, tunajua nchi nyingi zinatumia vitambulisho lakini kwa misingi ya haki sisi kwetu hakuna haki inayotendeka,” alisema Mkurugenzi huyo.

Alisema chama chake kinataka nchi za Ulaya, zifahamu kuwa Tanzania na hasa Zanzibar, hakuna demokrasia ya kweli wakati shughuli za uchaguzi zinazopoanza na kwamba kama nchi hizo zina uwezo wa kusaidia, zifanye hivyo ili haki itendeke.

Katika hatua nyingine, chama hicho kimeilalamikia Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), kwa kuhamisha vituo vyote vya uandikishaji katika Jimbo la Mtambwe na kuvipeleka katika Shule ya Daya,Kaskazini Pemba.

Mkurugenzi wa Oganaizesheni na uchaguzi wa chama hicho, Juma Said Sanani, aliwaambia waandishi wa habari kuwa awali vituo vilikuwa katika shule zilizoko ndani ya jimbo hilo na kwamba sasa ZEC imeamua kuvipeleka umbali wa zaidi ya kilomita nane,lengo likiwa ni kukidhoofisha chama chake na wananchi.

Alidaiu kuwa ZEC imefanya hivyo kwa makusudi ili kuwahangaisha wananchi wanaotaka kwenda kujiandikishwa.

“ZEC kwa makusudi imehamisha vituo vyote vya Jimbo la Mtambwe, na kuvipeleka skuli ya Daya ambako ni zaidi ya kilomita nane na wamefanya hivyo taarifa wala kujali kuwa kuna wazee wagonjwa na wasiojiweza, Tunajua kuwa huo ni mkakati maalumu wa kuidhoofisha CUF, “alisema.

Hata hivyo akizungumzia madai hayo, Mkurugenzi wa ZEC, Salim Kassim Ali, alisema hayana msingi hasa ikizingatiwa kuwa vyama vyote vilipewa ratiba ya uandikishaji.

“ZEC imevipatia vyama vyote vya siasa, ratiba ya uandikishaji na hadi sasa hatujapokea malalamiko yoyote kutoka katika chama chochote cha siasa, lakini kama kuna chama chenye malalamiko waje nayo badala ya kuzungumzia kupitia vyombo vya habari,”alisema.

Mkurugenzi huyo alisema kuvipeleka vituo katika shule ya Daya kumefanywa kwa sababu za kiusalama zaidi.

Chanzo: Mwananchi la 30 Septemba 2009

Advertisements

Actions

Information

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s
%d bloggers like this: