Zanzibar in the News

26 09 2009

Date::9/24/2009
Wakili: Vurugu Zanzibar hazitakoma kwa nguvu ya dola

Na Hussein Kauli
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) kimesema nguvu za kijeshi zinazotumiwa katika vurugu zinazoendelea kisiwani Zanzibar, haziwezi kuwa suluhisho la kudumu la matatizo yaliyopo kisiwani hapo.
Akizungumza ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Mwanasheria na Wakili wa kituo hicho, Clarence Kipobota, alisema hali hiyo imetokana na ukweli kwamba matatizo ya kisheria na hali ya kisiasa iliyopo katika kisiwa hicho ndio chanzo cha vurugu hizo.
“Matatizo ya kisheria na hali ya kisiasa iliyopo kisiwani Zanzibar, ndio chanzo kikubwa cha vurugo zinazoendelea huko, kwa hali hiyo huwezi kuzuia vurugu hizo kwa kuleta polisi”, alisema Kipobota.
Kipobota alisema kuwahusisha masheha katika masuala ya uchaguzi ndilo linalosababisha vurugu kwani, wale ni viongozi wa serikali wapo kwa maslahi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
“Pemba inakaliwa kwa asilimia kubwa na wafuasi wa vyama vya upinzani, kujiandikisha kwa wingi kwa wafuasi hao ni kuhatarisha uwepo wa Serikali ya Chama tawala. Kwa hali hiyo migogoro ni wazi inaweza kutokea”, aliongeza Kipobota.
Kutokana na hali hiyo ameomba serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kufanya marekebisho ya sheria ili kutowahusisha masheha katika masuala ya uchaguzi kama ilivyo bara.
Kwa upande wa hali ya kisiasa iliyopo kisiwani hapo, Kipobota, alipendekeza mazungumzo ya kutafuta muafaka yaimarishwe ili kuleta maelewano katika siasa za kisiwa hicho.
“Hali ya kisiasa iliyopo sasa, mtu akizungumza jambo, hata kama hakusudii vibaya linachukuliwa kiupinzani, hivyo kuzusha vurugu zisizo za msingi” alisema Kipobota na kuongeza:
“Ili kuondoa hali hiyo kunahitajika maelewano kwa viongozi na wafuasi wa kisiasa na hakuna njia ya kufikia huko zaidi ya kuendeleza mazungumzo ya muwafaka katika masuala hayo”.
Akizungumzia kauli ya Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar( Zec), Salum Kassim, kupinga hoja ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania (Nec), Jaji Lewis Makame kwamba, jamii iilaumu Zec kwa vurugu zinazoendelea kisiwani Pemba, Kipobota alisema Zec ndio wanastahili kubeba mzigo wa vurugu hizo na si Nec.
“Zec na Nec ni vyombo viwili ambavyo kila kimoja kinajitegemea, kuihusisha Nec kwenye vurugu za Zanzibar ni kusababisha mgogoro wa kiutendaji” alisema Kipobota na kuongeza:
“Zec haina namna ya kukwepa matatizo hayo, inachotakiwa kufanya ni kuhakikisha inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria ili kumaliza vurugu hizo.”
Kipobota alisema, Zanzibar ina watu wachache ambao ni sawa na mikoa miwili ya Tanzania bara, hivyo kitendo cha Zec kuonyesha imeshindwa kazi ni udhaifu wa kiutendaji.
“Nec kwa nafasi yao wangetakiwa wawe washauri wa masuala ya uchaguzi kisiwani Zanzibar na si kuingilia mambo yaliyo nje ya Jamhuri”

Tuma maoni kwa Mhariri
Facebook

Advertisements

Actions

Information

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s
%d bloggers like this: