Zaidi ya wanawake 1,300 wajiunga na kisomo cha watu wazima Zanzibar

23 09 2009

Mwandishi Maalumu

ZAIDI ya wanawake 1,317 kutoka Pemba Kaskazini na Kusini Unguja, wameanza kujua kusoma na kuandika baada ya kujiunga na mpango wa elimu ya watu wazima unaoendeshwa chini ya mradi wa kuwawezesha wanawake huko Zanzibar (Weza).

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa habari wanawake, Ananilea Nkya asilimia 75 ya wanawake walionufaika na mpango huo wa elimu ya watu wazima ulioanza Januari mwaka huu wanatoka Pemba na wengine asilimia 25 wanatoka Unguja.

Alisema kuwa katika kufanikisha jitihada za kuhakikisha kuwa wanawake waliojiunga na mradi wa Weza wanafahamu kusoma na kuandika, mradi unashirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Jukwaa la Wanawake Wasomi barani Afrika (Fawe).

Mradi wa Weza umeanzisha darasa la elimu ya watu wazima kwa wanawake wanaonufaika na mradi huo kutokana na kutambua kuwa rasilimali elimu ni nyenzo katika kuwezesha wanawake kunufaika na rasilimali nyingine muhimu za kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Wanawake hao walisema kuwa hivi sasa wataweza kusonga mbele kimaisha bila ya wasiwasi tofauti na mwanzo ambapo walikutana na vikwazo mbalimbali vinavyohusiana na kusoma na kuandika.

Mwamtoto Hamad (30) alisema kutokana na kutokujua kusoma aliwahi kuchukua daftari la mumewe la hospitali bila yeye kutambua na hivyo hakuweza kutibiwa baada ya kusubiri kuitwa kumuona daktari hadi muda kumalizika.

Karibu asilimia 95 ya wanawake wanatoka shehia ya Maziwa Ng’ombe Mkoa wa Pemba Kaskazini ambapo na watoto wao hawakupata elimu ya msingi kutokana na kutokuwepo shule katika Shehia hiyo.

Hidaya Hamza (28) kutoka shehia ya Kiuyu Minungwini alisema kujua kusoma na kuandika kutamuwezesha kuandaa maandiko mbalimbali na pia kuweza kuweka saini. “Ilikera sana awali kuwa siwezi hata kuweka saini yangu katika jambo linalonihusu”.

Hamza alisema alitambua kuwa elimu kwa wanawake na makundi mengine yaliyoko pembezoni ni rasilimali muhimu katika kutokomeza umaskini.
Chanzo: Mwananchi, 22 Septemba 2009

Advertisements

Actions

Information

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s
%d bloggers like this: