Kikundi Zanzibar chatishia kumshitaki Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

15 09 2009

Na Mwantanga Ame

MWENYEKITI wa kikundi kinachojiita Umoja wa Wazanzibari, Rashid Salum Adiy, ametishia kumshitaki Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) endapo hawatapatiwa majibu ya masuali kadhaa likiwemo nafasi ya Zanzibar katika umoja huo ndani ya siku 14. Rashid alitoa tahadhari hiyo jana alipozungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

Alisema tayari wametuma barua hiyo kwa Katibu Mkuu Ban Ki Moon kumueleza dhamira hiyo kupitia Kampuni ya J.C. CHIDZIPHA & CO. ADVOCATES waliyoipa kazi ya kuwatetea mahakamani watakapofungua kesi hiyo. Alisema barua imemtaka Ban Ki Moon kuelezea Mamlaka ya Zanzibar katika Umoja wa Mataifa iwapo bado ipo, na kama inaendelea kuwa mwanachama wa Umoja huo.

Aidha, lipo pia suala la Muungano wa Tanzania kujiunga na umoja huo kama Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikaa na kukubaliana na hayo. Majibu mengine wanayotaka kupatiwa ni kama Serikali ya Zanzibar iliwasilisha barua ya kukana uanachama wake na kama Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanganyika waliuthibitisha UN Muungano huo baada ya kutangazwa.

Jengine ni iwapo Zanzibar iliondoa uanachama wake; na iwapo serikali ya Muungano ilitangaza suala hilo katika gazeti rasmi la serikali na kukubaliwa. Aidha, wanahoji kama ulikuwepo utaratibu wa kukusanya maoni ya wananchi kwa mujibu wa sheria za ndani ya nchi kutaka kujiondoa katika umoja huo.

Alidai kuwa masuala hayo kwa UN yana lengo la kuweka misingi ya mambo yanayojitokeza katika kero za Muungano na ikiwa watashindwa kuyapatia ufumbuzi kampuni hiyo itafungua kesi hiyo rasmi mahakamani.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo muda walioutoa tayari umepita kwa kuwa barua hiyo ilitumwa tangu Agosti 18, 2009. Alisema matayarisho ya kesi hiyo yanaendelea na itawashirikisha mawakili kutoka Kenya, India na nchi za Magharibi; lakini hakutaja majina ya mawakili hao kwa madai kuwa kazi hiyo inafanywa na kampuni iliyotajwa.

Alifahamisha kuwa wameamua kufanya hivyo kwa kutambua kuwa wapo Wazanzibari wa ndani na nje ya nchi watakaowaunga mkono kuhusu suala hilo ingawa walikiri kutokua na idadi rasmi ya wanaowaunga mkono.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Brenden Varma, alipozungumza na Idara ya habari Maelezo ya Zanzibar tarehe 14 Juni 2006 alisema kwa mujibu wa kifungu cha 18 (a) cha sheria za Umoja huo za mwaka 1946 inayohusu haki na kinga dhidi ya mashtaka kwa Katibu Mkuu wa Umoja huo kimeeleza hatoweza kushtakiwa katibu Mkuu akiwa kazini. Varma alisema ili Katibu Mkuu huyo aweze kushtakiwa ni lazima aondoshiwe kinga aliyonayo; jambo ambalo si aghalabu kufanyika.

CHANZO: ZANZIBAR LEO

Advertisements

Actions

Information

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s
%d bloggers like this: