SMZ acheni kuishutumu Marekani jirekebisheni

2 09 2009

MAREKANI imewatahadharia raia wake kutopanga safari zisizo za lazima kwenda Pemba, baada ya kutokuwa na imani ya usalama katika eneo hilo wakati huu wa kuekea uchaguzi mkuu wa mwakani.
Pamoja na tahadhari hiyo, raia wa Marekani wanaofika nchini kwa ajili ya kwenda Zanzibar hutakiwa kufika kwanza katika ubalozi wa nchi hiyo uliopo Dar es Salaam ili kuhakikisha usalama wao wawapo nchini.
Hatua hiyo ya Marekani inashtua na inaitia doa si tu kwa Zanzibar, bali kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mbele ya jumuia ya kimaitaifa; hivyo kuleta athari kubwa za kiuchumi na kijamii. Ni dhahiri hatua hiyo, itaathiri kwa kiasi kikubwa utalii ambao ni moja ya nguzo za uchumi Zanzibar.
Si hivyo tu, katika mazingira ya aina hiyo, ni rahisi wageni kutoka Marekani na nchi nyingine duniani kuwa na mashaka na usalama wao wakija Tanzania; hivyo ni rahisi kubadili njia kwenda mahali pengine hadi watakaporidhika kuwa hali ni shwari.
Inasikitisha kuwa uamuzi huo mzito umeshafikiwa na taifa hilo, lakini kibaya zaidi ni pale juhudi za kurekebisha kasoro zinaposuasu, huku mamlaka husika zitoa kauli za kuilaumu Marekani badala ya kutafakri na kujisahihisha.
Mwezi uliopita mabalozi wa nchi za Jumuiya ya Ulaya (EU), Marekani na Canada walipo nchini walizitaka Serikali ya Muungano (SMT) na ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kuhakikisha kuwa matatizo yailiyojitokeza wakati wa zoezi la marekebisho ya Daftari la Kudumu la Wapigakura na kusababishwa vurugu kisiwani Pemba yarekebishwe.
Badala ya kuona kuwa huo ni ushauri mzuri; kiongozi mmoja wa SMZ aliitunisha misuli Marekeni na kuwaonya mabalozi hao wasiingilie mambo ya ndani ya nchi na kutamba kwamba, Zanzibar ni nchi huru yenye katiba yake.
Cha kushangaza, kauli hizo zimerudia tena juzi baada ya taarifa ya Marekeni kuwatahadharisha raia wake kutoenda Pemba kama ambavyo Naibu Waziri wan chi, Ofisi wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma alivyokaririwa na gazeti hili akiilamu nchi hiyo kuwa ina ajenda yake kwasababu Pemba hakuna tatizo lolote.
Ni vizuri SMZ wakawa wakweli kuhusu hali ya Pemba kwasababu kila mtu anajua vurugu zilitokea, ndiyo maana zoezi la uandishaji lilisimamishwa. Matukio kama hayo yanaashiria kuwa hali inaweza kwa mbaya hasa wakati kama huu.
Historia inaonyesha kuanzia 1995; wakati wa mchakato, uchaguzi na baada hapo kunakuwa na vurugu Zanzibar na hasa Pemba, zinazosababisha baadhi yao watu kujeruhiwa au kupoteza maisha yao. Tunaomba SMZ isiilamu Marekani bali ichukue hatua zinazostahili kufuta doa hilo.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Actions

Information

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s
%d bloggers like this: