Mifuko ya plastiki bado inatumiwa kinyemela Zanzibar

29 08 2009

Na Asha Haji, ZJMMC

BAADHI ya wafanyabiashara wa Zanzibar wameonekana kuendelea kuuza mifuko ya plastiki na kuupuza amri ya Serikali licha ya kupiga marufuku matumizi ya mifuko hiyo hapa nchini.
Hali hiyo imebainika kufuatia mwandishi wa habari hizi kutembelea katika maeneo tofauti ya biashara katika Manispaa ya mji wa Zanzibar na vitongoji vyake nakubaini kwamba katika maeneo mengi ya biashara bado inaendelea kutumika. Wafanyabaishara wadogo wadogo wanaoza bidhaa katika maeneo mbali mbali maarufu ya biashara mjini hapa wamekuwa wakiwatilia bidhaa wateja wao licha kwamba wamekuwa wakiificha mifuko hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mwanasheria kutoka Idara ya mazingira Saada Mussa Said, alithibitisha kuwepo kwa matumizi ya mifuko hiyo, ambapo alisema taasisi yake inaendelea na operesheni dhidi ya kupambana na wafanyabiashara wanaouza mifuko hiyo kwa wananchi katika masoko ya Darajani na Mwanakwerekwe. “Hivi sasa tumeshajipanga na tutafanya msako pia kwa siku za Jumamosi na Jumapili,” alisisitiza Mwanasheria huyo.

Aidha, Saada alisema Idara ya Mazingira ina mpango wa kuweka mabango ya kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki katika sehemu za bandarini na viwanja vya ndege ili kuhakikisha kuwa mifuko hiyo inatoweka kabisa. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Idara ya Mazingira ilipiga marufuku uingizaji, uuzaji na matumizi ya mifuko ya palastiki ya aina zote na tokea marufuku hiyo wafanyabiashara kadhaa wamekamatwa na kupelekwa mahakamani; lakini bado wanaendelea kutumia kwa njia za kificho.

Advertisements

Actions

Information

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s
%d bloggers like this: