Jumba la kulelea watoto Forodhani kugeuzwa makumbusho

29 08 2009

Na Mwanajuma Abdi, TSJ

JUMBA lililokuwa la kulelea watoto yatima Forodhani linatarajiwa kugeuzwa makumbusho ya usafiri wa baharini ili kutowa fursa kwa wageni na wenyeji kupata historia ya mambo hayo hapa Zanzibar. Jumba hilo, ambalo awali yake walikuwa wakiishi watoto yatima waliokuwa na uangalizi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambao kwa sasa wamehamia katika jengo jipya lililojengwa na Mke wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya ZAYEDESA, Mama Shadya Karume, huko Mazizini mjini hapa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mwalim Ali Mwalim, alisema kuwa mchakato unaendelea wa matayarisho ya kufanywa makumbusho jumba hilo. Alisema makumbusho hayo yatafanywa kwa ufadhili mkubwa na Aga Khan Trust Culture (AKTC), ambao ndio wamejotolea kusaidia kuwepo kwa makumbusho hayo, ambayo kwa muda mrefu yalikuwa yanahitajika kuwepo hapa Zanzibar. Alieleza kuwa licha ya Aga Khan kujitolea kufanya makumbusho hayo, lakini intaendelea kubakia kuwa ni mali ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Akizungumzia mradi wa huduma za mijini (Urban Service project ), alisema mradi huo utakuwa na sehemu mbili, ikiwemo ya uwekaji wa taa za barabarani katika maeneo yote ya mijini Zanzibar; na awamu ya pili ni ujenzi wa ukuta na utanuzi wa barabara ya Forodhani ili kutoa nafasi nzuri kwa vyombo vya usafiri ardhini na wapitao kwa miguu. Alizidi kufahamisha kuwa utiaji saini wa makubaliano ya ujenzi huo umeshafanyika na Benki ya Dunia mwaka huu; ila kinachosubiriwa ni kupatikana kwa kampuni itakayobahatika kujenga.
Alisema kuwa mchakato wa kutayarisha michoro ya ramani pamoja na zabuni unaendelea Serikalini kwa lengo la kuhakikisha kwamba azma hiyo inatimizwa kwa wakati unaofaa.

CHANZO: ZANZIBAR LEO

Advertisements

Actions

Information

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s
%d bloggers like this: