Bodi yabaini maziwa yasiyofaa kuwepo Zanzibar

29 08 2009

Na Mwantanga Ame

BODI ya Udhibiti wa Dawa, Vyakula na Vipodozi Zanzibar imefanya msako wa kushitukiza katika maduka mbali mbali kutafuta maziwa aina ya S26 yanayosadikiwa hayafai kwa matumizi ya binadamu. Bodi hiyo katika msako huo pia imefanikiwa kukamata kiwango kidogo cha maziwa na imeyapiga marufuku kuuzwa na kutumiwa na wananchi Zanzibar.
Msako huo ulifanyika jana katika maduka tofautio mjini hapa baada ya kubainika kuwapo maziwa hayo yenye namba moja chini ya jina lake yanayoaminika kuwa na athari kwa wanaoyatumia; hasa watoto.

Inaaminika kuwa maziwa hayo yaliingizwa Zanzibar na wafanya biashara tofauti hapa nchini kwa muda sasa yakitokea nchini Afrika ya Kusini ambako ndiko yalikotengenezwa.
Maeneo yaliyohusika na msako huo ni Darajani, Mpendae, Chukwani na Kiembesamaki, katika Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.

Hii ni mara ya pili kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Zanzibar kuchukua hatua ya kupiga marufuku kuingizwa bidhaa za aina hiyo nchini baada ya tahadhari iliyotolewa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO). Aidha maziwa hayo yalibainika kuwa na kemikali kwa kuingizwa Protini za kutengenezwa katika maziwa ya Lactogen 1. Tamko hilo la WHO lilikuja baada ya Wizara ya Afya nchini China kubaini kuwapo kwa maziwa yaliokuwa na kemikali aina ya Melamini zenye madhara kwa watoto ambapo zaidi ya watoto 100 waliotumia maziwa hayo waliathirika kwa kupata vijiwe tumboni. Aidha, serikali ya nchi hiyo iliamua kukifunga kiwanda kilichokuwa kikizalisha maziwa hayo kulinda usalama wa afya za wananchi wake na soko lake la biashara duniani.

Kaimu Mrajis wa Kitengo hicho, Haji Ameir Bonde, alilithibitisha kufanyika msako huo baada ya Ofisi yake kupata taarifa hizo kutoka kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Tanzania (TFBA). Alisema Mamlaka hiyo ilibaini maziwa hayo yaliyokuwa sokoni kwamba yameharibika na kuagizwa kufanywa uchunguzi hapa Zanzibar ili kuthibitisha iwapo kuna bidhaa za aina hiyo na SMZ iyapige marufuku. Alisema uchunguzi ulibaini kuwepo maziwa hayo katika maduka ya mji wa Zanzibar na walipoyachunguza wamegundua kuwa na athari kwa matumizi ya binadamu na hayafai kuendelea kutumika hapa nchini.

Mrajis huyo alisema kilichobainika ndani ya maziwa hayo ni kiwango kilichopita cha ‘Free Faty Acid’ (FFA), kemikali ambayo imebainika kuwemo katika maziwa hayo pamoja na Peroxide ambazo dalili zake zimeonesha kuharibika. Mbali ya kuwa na kemikali hiyo, pia maziwa hayo yamebainika kwamba hayayuki katika mchanganyiko wake; na pia yanatoa harufu mbaya.

Aidha, imebainika kuwa maziwa hayo yanaweza kuwasababishia athari mbaya watumiaji hasa watoto kwa kupata matatizo ya ugonjwa wa kuharisha, kwenda chafya kwa wingi, tatizo la kizunguzungu na kutapika. Alisema maziwa hayo yanatambulika kutokana na kuhifadhiwa katika makopo yenye mfuniko na ukanda wa juu wa buluu na katika eneo lake la makalio ukanda wake una rangi ya waridi. Alifahamisha kuwa jina halisi la maziwa hayo ni S26, ikiwa na namba moja yaliotengenezwa na kiwanda cha ‘Pharmcare Ltd Building 12 Health care park, Wood mead, Santon’ ya Afrika kusini.

Aliongeza kuwa katika msako walioufanya wamefanikiwa kukamata makopo 38 yenye ujazo wa gramu 400 kwa kila moja na huuzwa zaidi kwa matumizi ya watoto. Alisema kumbumbukumbu zinaonesha kuwa maziwa hayo yalitengenezwa mwezi Agosti mwaka jana na yalitarajiwa kumaliza muda wa matumizi mnamo mwezi Agosti mwakani; lakini yaliharibika yakiwa bado sokoni. Alisema msako wakutafuta maziwa hayo unaendelea katika maduka ya mitaa ya Mwembenjugu, Mwanakwerekwe na Amani.

Hata hivyo, Mrajis huyo alisema sio maziwa yote ya Kampuni hiyo yaliopigwa marufuku kwani aina nyengine ya maziwa hayo bado yapo salama. Alisema wananchi wanalazimika kuwa makini wanapokwenda madukani kununua bidhaa hiyo kwa lengo la kuepuka kununua yale yenye athari kwa afya za binaadamu. “Sio maziwa yote ya S26 yenye matatizo haya lakini jamii itapaswa kuwa makini kuangalia hizi rangi tulizozionesha zilivyo kwenye makopo yake na mzalishaji”, alisema. Alionya kuwa mfanyabishara ambaye hatatoa ushirikiano wa kuweka hadharani bidhaa zake, yakiwemo maziwa hayo, akibainika atachukuliwa hatua za kisheria.

Chanzo: Zanzibar Leo

Advertisements

Actions

Information

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s
%d bloggers like this: